Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2020

UNENE ULIOPITILIZA

  Unene Uliopitiliza (Obesity) Tatizo la Unene Uliopitiliza (Obesity) Tatizo hili la unene uliopitiliza kuliko inavyohitajika kiafya huwa linaletwa na kuongezeka kwa kiwango cha mafuta mwilini. Njia rahisi na inayokubalika ya kuweza kugundua kama mtu ni mnene kupita kiasi (obese) inafahamika kama kipimo cha Body Mass Index (BMI). Vipimo hivi vya BMI ndio vinaweza kukujulisha kama unene ulionao unastahili kulingana na umri, urefu na uzito wako. Vipimo hivi ni kama ifuatavyo: Jinsi ya kupima BMI yako Kanuni ya BMI hutumia uzito wa mtu pamoja na urefu wake. Uzito wa mtu hupimwa katika kilograms (kg) na urefu wake katika mita (m) au sentimita (cm). Ikumbukwe pia kuwa mita moja ni sawa na sentimita 100 na mita² = mita x mita. Category BMI range – kg/m2 Emaciation less than 14.9 Underweight from 15 to 18.4 Normal from 18.5 to 22.9 Overweight from 23 to 27.5 Obese from 27.6 to 40 Morbidly Obese greater than 40 BMI (kg/m2) = Uzito katika kilograms/Urefu katika meters². Maana yake ni kwamba...

LOW OR LOSS OF SEXUAL LIBIDO

  Kupungua au Kukosa Hamu ya Kufanya Mapenzi (Low or Loss of Sexual Libido) Matatizo ya kukosa au kupungua hamu ya kujamiana yanatambulika kama tatizo linalojirudia kwa muda mrefu ambapo huathiri mzunguko wa tendo la kujamiana (kusisimka, kufikia kilele, kurudia) na hivyo kusababisha msongo wa mawazo au kuharibu uhusiano kati ya mtu na mwenza wake. Katika makala hii, mwandishi wako DkThobiasBedavitu vinavyoweza kusababisha tatizo hili na jinsi ya kuliepuka. Kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi ni suala linaloonekana kuathiri wenza wengi. Jamii imeshuhudia visa vingi vinavyosababishwa na mwenza mmoja kutoka nje ya ndoa au uhusiano kwa kisingizio cha kutoridhishwa na utendaji wa mwenzake katika suala la kujamiana. Kadhalika jambo hili limesababisha kuvurugika kwa ndoa nyingi na wakati mwingine kusababisha magonjwa au hata vifo kwa mmoja au wenza wote wawili. Lakini nini hasa sababu ya kuwepo kwake? Kwa ujumla visababishi vya tatizo hili kwa wanaume na wanawake ni pamoja na mson...

MAGONJWA YA ZINAA

  Ugonjwa wa Trichomoniasis ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya jamii ya protozoan vinavyojulikana kama Trichomonas vaginalis. Ugonjwa huu huathiri mrija wa kupitisha mkojo unaojulikana kama urethra na tupu ya mwanamke (vagina). Trichomoniasis pia hujulikana kwa majina mengine kama Trichomonas vaginitis au Trich (tamka “Trick”). Trichomoniasis huathiri watu milioni 8 kwa mwaka Nchini Marekani na watu milioni 170 kwa mwaka dunia nzima. Ugonjwa huu huonekana sana kwa wanawake kuliko wanaume labda kutokana na wanaume kutoonyesha dalili zozote wakati wa maambukizi au kutokana na majimaji ya kwenye tezi dume kuwa na madini ya zinc ambayo huathiri vimelea hivi vya Trichomonas vaginalis. Ugonjwa huu hupatikana kwa njia ya kujamiana bila kutumia kinga na mtu aliyeathirika na Trichomoniasis. Nakumbuka mwanajumuiya mmoja wa TanzMed aliuliza swali na hapa naomba ninukuu “madaktari, poleni na kazi za kila siku. mimi nina tatizo napata sana hizi yellowish discharge au niseme kama rangi ya ...

MAMBO MAKUU 5 UNAYOTAKIWA KUJUA KUHUSIANA NA HEDHI YAKO

  Je unafahamu inakadiriwa kuwa, mwanamke hupata hedhi wastani wa mara 400 katika maisha yake? Pia, neno linalotumika sana kuwakilisha hedhi ni "period", neno hili lilianza kutumika kwa mara ya kwanza kwenye miaka ya 1822 likimaanisha tukio linalotokea ndani ya muda fulani au linalojirudia baada ya muda fulani. Leo hii tuangalie mambo mengine 5 muhimu kuyajua kuhusiana na hedhi. 1. Kwa wastani, mwanamke huanza kupata hedhi yake ya kwanza kabisa akiwa na umri wa miaka 12. 2. Mzunguko wa siku za hedhi huwa kati ya siku 21 hadi 35. Ingawa wengi huwa na mzunguko wa siku 28, lakini kuzidi wiki moja au kuwahi kwa wiki moja ni kitu cha kawaida. 3. Mwanamke huzaliwa na mayai milioni 1 hadi 2. Mayai haya, mengi hufa jinsi mwanamke anavyoendelea kuishi na ni mayai 400 tu ndiyo hukadiriwa kufika hatua ya ukomavu tayari kwa uchavushwaji. 4. Msichana anaweza kupata ujauzito kabla ya kuanza hedhi yake ya kwanza. Hii ni kwa sababu, yai huanza kukomaa kabla ya kuona hedhi yake ya kwanza,...

MOYO

Moyo ni ogani ya mwili inayoendesha mzunguko wa damu mwilini. Kazi yake ni kama pampu ya damu. Hali halisi ni misuli inayosukuma damu kwenye mishipa kwa njia ya kujikaza. Mioyo ya mamalia pamoja na binadamu huwa na pande mbili. Upande wa kulia unasukuma damu kwenda mapafu inapopokea oksijeni; upande wa kushoto unazungusha damu katika sehemu nyingine za mwili pale ambako oksijeni inahitajika. Moyo ni ogani ya lazima kwa uhai. Moyo na utamaduni Katika masimulizi ya mataifa mengi moyo unajadiliwa kama mahali pa roho, mawazo au hisia, hasa pendo na chuki. Sababu yake ni kwamba pigo la moyo ni dalili ya wazi ya uhai na bila pigo la moyo mtu amekufa, kwa hiyo moyo ulitazamwa kama mahali pa uhai wenyewe pamoja na nafsi ya mtu. Siku hizi wataalamu wanaona moyo ni pampu tu, ni zaidi ubongo mahali pa nafsi ya mtu. Moyo unazungusha damu mwilini. Damu isiyo na oksijeni inafika moyoni (kulia) kutoka viungo. (na. 1+13) Moyo unapeleka damu hii kwenye mapafu inapoongezwa o...