Ruka hadi kwenye maudhui makuu

UNENE ULIOPITILIZA

 Unene Uliopitiliza (Obesity)

Unene Uliopitiliza (Obesity)



Tatizo la Unene Uliopitiliza (Obesity)

Tatizo hili la unene uliopitiliza kuliko inavyohitajika kiafya huwa linaletwa na kuongezeka kwa kiwango cha mafuta mwilini. Njia rahisi na inayokubalika ya kuweza kugundua kama mtu ni mnene kupita kiasi (obese) inafahamika kama kipimo cha Body Mass Index (BMI). Vipimo hivi vya BMI ndio vinaweza kukujulisha kama unene ulionao unastahili kulingana na umri, urefu na uzito wako. Vipimo hivi ni kama ifuatavyo:

Jinsi ya kupima BMI yako

Kanuni ya BMI hutumia uzito wa mtu pamoja na urefu wake. Uzito wa mtu hupimwa katika kilograms (kg) na urefu wake katika mita (m) au sentimita (cm). Ikumbukwe pia kuwa mita moja ni sawa na sentimita 100 na mita² = mita x mita.

CategoryBMI range – kg/m2
Emaciationless than 14.9
Underweightfrom 15 to 18.4
Normalfrom 18.5 to 22.9
Overweightfrom 23 to 27.5
Obesefrom 27.6 to 40
Morbidly Obesegreater than 40

BMI (kg/m2) = Uzito katika kilograms/Urefu katika meters². Maana yake ni kwamba ili kuweza kupata BMI itakayokuwezesha kujifahamu kama u mnene ama la, chukua uzito wako gawa kwa kipeo cha pili cha urefu wako.

Tatizo la unene uliopitiliza husababishwa na nini ?

Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha unene uliopitiliza. Mambo hayo ni pamoja na

  • Vyakula vya mafuta - Ulaji wa vyakula venye mafuta mengi au calories nyingi.
  • Kutofanya mazoezi - Wale wasiofanya mazoezi mara kwa mara huwa wanene tofauti na wale wanaofanya mazoezi.
  • Kurithi viashiria vya asili (genes) - Viashiria hivi vinaweza kuwa moja ya vichocheo vya kuongeza uzito kwani ndivyo huamua wapi mafuta huhifadhiwa mwilini na kwa kiwango gani. Lakini haimanishi kuwa mtu akiwa navyo basi ndio atakumbwa na tatizo hili.
  • Umri - Watu wengi huongezeka uzito au hunenepa kadri umri unavyoongezeka kwa sababu wanakuwa hawajishughulishi sana (less active) na huwa wanapungua maumbile ya miili yao (muscles mass)
  • Matatizo ya kisaikolojia - Wakati mwengine watu wenye matatizo ya kisaikolojia au msongo wa mawazo (stress) huwa na tabia ya kula sana, matokeo yake ni kunenepa.
  • Dawa - Baadhi ya dawa zenye madhara ya kuongeza unene ni kama corticosteroids, blood pressure medications, tricyclic medications na kadhalika.
  • Matatizo ya afya - Baadhi ya magonjwa yanachangia kuongezeka kwa uzito au kenenepa kama cushings syndrome, hypothyroidism, osteoarthritis na kadhalika

Vihatarishi vya tatizo la unene wa kupitiliza

Aidha yapo mambo kadhaa ambayo yanaweza kumuhatarisha mtu kupata unene wa kupitiliza. Mambo haya ni pamoja na

  • Kukua kwa uchumi wa nchi - Wananchi wengi wanaoishi kwenye nchi zilizoendelea au wenye kipato kikubwa ndio wanaopata tatizo hili kutokana na kuishi mfumo wa maisha ya kivivu na hali ya kutokufanya mazoezi (sedentary lifestyle).
  • Historia ya kuongezeka uzito uliopitiliza kwenye familia nayo yaweza kuhatarisha mtu kupata tatizo hili. Aidha, si jambo la kushangaza kuona karibu familia nzima au wengi wa wanafamilia kuwa wanene kupitiliza.
  • Kutojishughulisha na chochote (inactive).
  • Kupenda kula sana kuliko kawaida (overeating).
  • Kula vyakula vya mafuta mengi
  • Kutumia dawa zenye madhara ya kuongeza uzito uliopitiliza.
  • Kuwa na ugonjwa wa vichocheo mwilini (hormonal disorders) kama cushing syndrome, hypothyroidism.
  • Kuwa na msongo wa mawazo au kuathirika kisaikolojia.

Magonjwa yanaoweza kuambatana na tatizo la unene uliopitiliza

  • Kisukari
  • Shinikizo la damu (hypertension)
  • Kiharusi (Stroke)
  • Magonjwa ya moyo
  • Tatizo la kutopumua vizuri wakati mtu yupo usingizini (Sleep apnea)
  • Vijiwe katika mfuko wa nyongo (Gallstones)
  • Kiwango cha juu cha lijamu kwenye damu (cholesterol ikiwemo triglycerides)
  • Ugonjwa wa mifupa kama yabisi (osteoarthritis).
  • Saratani ya matiti
  • Saratani ya tezi dume (prostate cancer)
  • Saratani ya utumbo mpana pamoja na maeneo ya haja kubwa (Colorectal cancer)
  • Matatizo ya mzunguko na mishipa ya damu kama vile kuvimba kwa vena za miguuni (varicose veins)

Tiba ya kuongezeka unene kupita kiasi

Tiba ya tatizo hili ni mhusika kujitambua ya kwamba ana tatizo na kuwa tayari kupunguza uzito. Mabadiliko ya tabia ya mhusika ni muhimu sana, mabidiliko haya yawe ndio mfumo wa maisha yake ya kila siku.

Kupungua uzito na kujilinda au kutunza uzito ulionao baada ya kupunguza uzito ni jambo la msingi sana na inahusisha mazoezi, chakula na madiliko ya tabia ya mtu.

  • Mabadiliko ya tabia - Hii inahusisha muhusika kupunguza kiwango cha chakula anachokula lakini kiwe chenye virutubisho vyote muhimu vya afya na kuongeza kiwango cha ufanyaji mazoezi.
  • Mazoezi - Mazoezi husaidia kupunguza uzito hasa kipindi cha miezi sita ya mwanzo na hutunza uzito uliokusudiwa kwa muda mrefu. Pia hupunguza mafuta ya mwilini, huongeza ufanisi wa moyo, hupunguza tatizo la shinikizo la damu (hypertension), na kuweka sukari katika kiwango kinachohitajika mwilini.

Kama hujazoea kufanya mazoezi ni vizuri uanze taratibu na ujiwekee lengo kwa kufanya mazoezi kwa muda wa nusu saa kila siku, siku tano kwa wiki,(dakika 30 kila siku kwa siku tano kwa wiki). Mazoezi mazuri ni kama kuogelea, kuendesha baiskeli, kutembea, kunyanyua vitu vizito (visiwe vyenye uzito mkubwa), mazoezi ya viungo na kadhalika. Kama mtu ni mnene sana basi ni bora kuzungumza na daktari wako kabla ya kuanza mazoezi mapya. Baada ya kuanza mazoezi kwa mara ya kwanza, mwili utakuwa na maumivu, hii ni kawaida lakini kama mtu atapata maumivu zaidi ya masaa 2 baada ya kufanya mazoezi ni vizuri kumuona daktari.

  • Dawa - Zipo dawa nyingi za kupunguza uzito lakini ikumbukwe ya kwamba hakuna tiba ya tatizo hili na dawa hizi zina madhara mengi kama kuongeza shinikizo la damu (hypertension), matatizo ya moyo, kuharisha,msongo wa mawazo (depression) na mengineyo.
  • Chakula - Msingi wa kupunguza uzito au unene ni kujua ni kiwango gani cha calories mwili wako unahitaji kwa siku ili uwe unakula chakula ambacho hakitazidisha au kupunguza kiwango cha calories unazohitaji kwa siku. Mlo mzuri ni ule ulio na matunda kwa wingi, mboga za majani, nafaka ambazo hazijakobolewa, mafuta kidogo (less saturated fat). Vyakula vengine ni kama mayai, nyama isiokuwa ya mafuta (lean meat), samaki, kuku na vingineyo.
  • Tiba ya upasuaji - Kuna aina nyingi za upasuaji ambao unasaidia kupunguza uzito aina hizi ni kama gastric banding, gastric bypass (Roux-en-Y-procedure), liposuction. Kabla ya kufanyiwa upasuaji, muhusika atahitaji kupimwa kisaikolojia (psychological testing) na kupewa ushauri nasaha kwani tiba hii pia ina madhara yake.

Wanawake ambao wana uzito wa kupitiliza (obese women) wakiwa wajawazito wako kwenye hatari ya kupata madhara yafuatayo

  • Kisukari cha mimba (Gestatitional diabetes) - kisukari hiki kinatokea wakati wa ujauzito na hupotea baada ya kujifungua mtoto.
  • Shinikizo la damu (hypertension)
  • Shinikizo la damu wakati wa ujauzito pamoja na kifafa cha mimba (pre-eclampsia & eclampsia)
  • Kuzaa kwa njia ya upasuaji (caesarean section)
  • Tatizo la kiumbe kutopata hewa vizuri wakati wa ujauzito (fetal distress)

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

YOU HAVE A BRIGHT FUTURE. IF YOU WILL GIVE YOUR EARTHLY LIFE TO JESUS

https://mbochiherbal.blogspot.com But if you contract HIV you need to think through what you need to change in your life and then set to work to rebuild your immune system

WATU WA KALE WALIAMINI TANGAWIZI NI TIBA ZAIDI MAANA ILITIUBU MARADHI 28

WATU WAKALE WALITUMIA ZAO LA TANGAWIZI KAMA TIBA KWA KUTIBU TAKRIBANI MAGONJWA 28 NA 100% WALIPONA Tangawizi (kwa Kilatini zingiberis rhizoma; kwa Kiingereza: ginger) ni mzizi wa mtangawizi. Umbo la tangawizi ni kama lile la mzizi wa manjano na yote miwili hutumika kama viungo katika chakula. TANGAWIZI NI TIBA KUBWA IKITUMIWA VEMA Tangawizi huwa na utomvu wenye mafuta na kampaundi zinazofanya ukali wake. Utafiti wa kisasa umegundua tangawizi inaweza kusaidia katika matatizo ya utumbo na kuzuia kutapika Tangawizi inatazamiwa kupunguza maumivu ya viungo vilivyoathiriwa na rumatizimu na homa ya baridi yabisi (arthritis) KWENYE ELIMU YA KALE WALITUMIA TANGAWIZI KUJENGA AFYA Katika elimu ya tiba ya kale tangawizi ilitazamiwa kuwa na tabia nyingi za kujenga afya, lakini matokeo mengi yanayodaiwa mwilini hayajathibitishwa kisayansi: Imedaiwa kuwa na uwezo ufuatao wa kitiba: 1. kuondoa sumu mwilini Sumu ni dutu yoyote inayoweza kuharibu kiasi kidogo shughuli za seli au inayo...

TIBA YA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU

Shinikizo la juu la damu Shinikizo la juu la damu (HTN) au presha ya juu ya damu (pia huitwa shinikizo la mishipa ya damu , HBP), ni ugonjwa sugu ambapo nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ni kubwa kuliko kawaida. Ongezeko hilo husababisha moyo kufanya kazi kupita kiasi ili uzungushe damu katika mishipa ya damu. Kwa kawaida halina dalili, ila likidumu lina madhara makubwa kwa afya. Shinikizo la juu la damu ndilo sababu kubwa (kihatarishi) ya upoozaji, mshtuko wa moyo (mashambulizi ya moyo), moyo kushindwa kufanya kazi, kutuna kwa ukuta wa mishipa (k.m., kutuna kwa ukuta wa aota au mkole), chujio la mshipa wa kupeleka damu kwenye moyo au peripheral arterial disease, na inasababishwa na ugonjwa sugu wa figo. Hata ongezeko la wastani la shinikizo la damu hupunguza matarajio ya muda wa kuishi. Kuna vipimo viwili vya shinikizo la damu, yaani systolic na diastolic: shinikizo au presha ya systolic ni kipimo cha damu ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu katika mish...