Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAAMBUKIZI KWENYE NJIA YA MKOJO

     MAAMBUKIZI YA NJIA YA MKOJO



TATIZO LA TEZI KIBOFU, MAZOEZI, VYAKULA NA NJIA ZA KUJIHAMI… | kitoto


  ni maambukizi ya bakteria katika njia za mkojo. Yanapoathiri sehemu ya chini ya njia hizo, maambukizi hayo hujulikana kama sisititisi ndogo (maambukizi ya kibofu). Yanapoathiri sehemu ya juu ya njia za mkojo, maambukizi hayo hujulikana kama pilonifritisi (maambukizi ya figo).
Dalili katika sehemu ya chini ya njia za mkojo ni pamoja na uchungu wakati wa kukojoa na aidha kukojoa kila mara au kuhisi haja ya kukojoa (au zote mbili). Dalili za maambukizi ya figo huhusisha pia homa na maumivu ya fumbatio (mwanya wa fupanyonga). Katika wazee na watoto wachanga, dalili haziwi wazi kila wakati. Kisababishi kikuu cha aina hizo mbili niEscherichia coli. Hata hivyo, katika matukio machache, bakteria wengineo, virusi au kuvu wanaweza kuwa ndivyo visababishi.
Maambukizi ya njia za mkojo huwatokea mara nyingi zaidi wanawake kuliko wanaume. Nusu ya idadi ya wanawake huambukizwa wakati fulani maishani mwao. Marudio hutokea mara nyingi. Vipengele visababishi vilivyo hatari ni pamoja na ngono na pia historia ya kifamilia. Maambukizi ya figo yanaweza kufuatia maambukizi ya kibofu. Maambukizi ya figo pia yanaweza kusababishwa na maambukizi ya damu.

Utambuzi katika wanawake wachanga wenye afya unaweza kutazamwa kwa msingi wa dalili pekee. Utambuzi unaweza kuwa mgumu kwa watu walio na dalili zisizo wazi kwani bakteria wanaweza kuwepo hata kama mtu huyu hana maambukizi. Katika matukio yenye matatizo au ikiwa matibabu hayajafaulu, uchunguzi wa vimelea katika mkojo wakati mwingine husaidia. Mtu aliye na maambukizi ya kila mara anaweza kutumia kipimo kidogo cha antibiotiki kama namna ya kuzuia.
Matukio madogo ya maambukizi katika njia za mkojo hutibiwa kwa urahisi kwa kutumia mfululizo wa antibiotiki. Hata hivyo usugu dhidi ya antibiotiki zinazotumika kutibu hali hii, unaendelea kuongezeka. Watu walio na matukio yenye matatizo, wakati mwingine hushurutika kutumia antibiotiki kwa muda mrefu zaidi au watumie antibiotiki zinazodungwa ndani ya misuli. Ikiwa dalili hazipungui baada ya siku mbili au tatu, mtu atahitaji kufanyiwa uchunguzi zaidi. Katika wanawake, maambukizi ya njia za mkojo ndiyo maambukizi yanayotokea mara nyingi zaidi katika aina zote za maambukizi ya bakteria. Asilimia kumi ya wanawake hupata maambukizi ya nia za mkojo kila mwaka.




Dalili na ishara


Mkojo unaweza kuwa na usaha (hali inayojulikana kama piuria) kama inavyoonekana katika mtu aliye na sepsisikufuatia maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo.
Maambukizi ya sehemu ya chini ya mfumo wa viungo vya mkojo pia hujulikana kama maambukizi ya kibofu. Dalili zinazotokea mara nyingi zaidi ni hisia za kuchomeka wakati wa kukojoa na kukojoa kila mara (au kuhisi kukojoa) bila mchozo wa uke na maumivu mengi. Dalili hizi zinaweza kutofautiana kutoka dalili zisizo kali hadi dalili kali. Katika wanawake wenye afya njema, dalili hizi hudumu kwa wastani siku sita. Baadhi ya watu huwa na maumivu juu ya mfupa wa kinene au kwenye maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo. Watu walio na maambukizi katika sehemu ya juu ya mfumo wa viungo vya mkojo au pilonifritisi (maambukizi ya figo), wanaweza kuwa na maumivu katika maumivu ya fupanyonga, homa au kichefuchefu na kutapika. Dalili hizi huambatana na kikundi cha dalili za maambukizi ya upande wa chini cha mfumo wa viungo vya mkojo. Mkojo huwa na damu mara nadra sana au kuwa na piuria (usaha katika mkojo).

   kwa watoto

Katika watoto wachanga, dalili pekee ya maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo yanaweza kuwa homa.. Mashirika mengi ya afya hupendekeza uchunguzi wa vimelea katika mkojo wakati wasichana wa chini ya umri wa miaka miwili au vijana ambao hawajatahiriwa walio wa chini ya umri wa mwaka mmoja wanapopata homa. Watoto wachanga walio na maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo wakati mwingine hukumbwa na ugumu wa kula kutapika, hulala sana au kuonyesha dalili za umanjano. Watoto wakubwa wanaweza kukumbwa na kutoweza kujizuia kukojoa kwa ghafla (kupoteza udhibiti wa kibofu).

                  wazee

Dalili za mfumo wa viungo vya mkojo zinakosekana mara nyingi katika uzee. Wakati mwingine, dalili pekee ufukunyungu (kutoweza kujizuia kukojoa) mabadiliko katika hali ya kiakili, au uchovu]Dalili ya kwanza katika watu wazee ni sepsisi, ambayo ni maambukizi ya damu Utambuzi unaweza kutatizika kwa sababu watu wengi wazee wana ufukunyungu au wana dimenshia wana (hali lemavu ya kiakili).

Kisababishi

E. coli ndicho kisababishi cha asilimia 80–85 ya maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo. Staphylococcus saprophyticus ndicho kisababishi cha asilimia 5–10 ya matukio haya. Kwa nadra sana, maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo husababishwa na maambukizi virusi au kuvu. Visababishi vya kibakteria ni pamoja na:Klebsiella, Proteus, Pseudomonas, na Enterobacter.Visababishi vya kibakteria huwa havitokei mara nyingi na kwa kawaida huhusishwa na hali zisizo za kawaida za mfumo wa viungo vya mkojo au kuweka katheta kwenye mfumo wa viungo vya mkojo.[3] Maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo yanayosababishwa naStaphylococcus aureus kwa kawaida hutokea kufuatia maambukizi yanayotokana na damu.

Jinsia

Ngono husababisha asilimia 75–90 ya maambukizi ya kibofu katika wanawake wadogo wanaojihusisha na ngono sana. Hatari ya kuambukizwa huhusishwa na idadi ya marudio ya ngono.Huku maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo yakitokea mara vyingi wakati wanawake wanapoolewa, tamko sisititisi ya fungate" hutumika mara nyingi. Katika wanawake walio katika baada ya ukomo hedhi ngono haiathiri hatari ya kupata maambukizi ya mfumo ya viungo vya mkojoMatumizi ya spemisidi huongeza hatari ya maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo.
Wanawake hupata maambukizi mengi zaidi ya mfumo wa viungo vya mkojo kwa sababu wao wana urethra fupi na iliyo karibu na kinyeo. Huku kiwango cha estrojeni ya wanawake (homoni) kinaposhuka kufuatia ukomohedhi, hatari ya maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo hupanda kwa sababu ya kupoteza flora ya uke inayokinga (bakteria njema iliyo ukeni).

Katheta za mkojo

Kuweka katheta kwenye mfumo wa viungo vya mkojo huongeza hatari ya maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo. Hatari ya bakteriuria(bakteria kwenye mkojo) ni asilimia 3 hadi 6 kila siku. Antibiotiki haifaulu katika kuzuia maambukizi. Hatari ya maambukizi husika inaweza kupunguzwa kwa kutumia katheta inapohitajika, kwa kutumia ufundisanifu usio na bakteria kuingiza katheta na kuhakikisha kuwa katheta hii inavuta mkojo bila kuzibika.

Nyingine

Maambukizi ya kibofu ni ya kawaida sana katika familia zingine.. Sababu zingine za hatari ni pamoja na kisukari, kuwa asiyetahiriwa, na kuwa na haipatrofia hafifu ya kibofu|kibofu kinene] Vipengele vinavyochangia matatizo havijulikani vyema. Vipengele hivi ni pamoja na matatizo hatarishi ya kianatomia (yanaohusiana na muundo wa kimwili), kiutumizi au kiumetaboli.. Maambukizi tata ya mfumo wa viungo vya mkojo huwa magumu kutibu na huhitaji utathmini, matibabu na ufuatilizi wa kina zaidi.  Katika watoto, maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo huhusishwa namrejeo wa kiboofuni na ureta (mwendo usio wa kawaida wamkojo kutoka katika kibofu hadiuretaau figo nakufungika kwa choo.

Pathogenesisi

Bakteria inayosababisha maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo huingia kibofuni kupitika urethra. Hata hivyo, maambukizi yanaweza kuingia kupitia damu au limfu. Madaktari wanaamini kuwa bakteria hii huingia katika urethra kutoka matumboni. Wanawake wako katika hatari kuu zaidi kwa sababu ya maumbile ya viungo vyao vya ndani. Baada ya kuingia katika kibofu, bakteria zaE. Coli zina uwezo wa kujibandika katika pembezo mwa kibofu na kuunda bayofilamu (mpako wa vidubini) inayopinga mwitikio wa kingamwili.

Kinga

Idadi kubwa ya njia za kukinga hazijathibitishwa kubadili matokeo ya mara nyingi ya maabukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo. Njia hizi ni pamoja na tembe za kuzuia mimba au kondomu, kukojoa punde baada ya ngono, aina ya chupi iliyotumiwa, mbinu za usafi wa kibnafsi zinazotumika baada ya kukojoa au kukunya, au kama mtu kwa kawaida huoga kwa karai au mfereji. Vilevile, hakuna ushahidi wa kutosheleza kyuonyesha kuwa kukawisha mkojo, kutumia kisodo na kuonya uke kwa maji mengi kunaweza kusababisha maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo.
Watu wanaoambukizwa mara kwa mara na pia kutumia spemisidi au kiwambo kama njia ya kuzuia mimba wanashauriwa kutumia mbinu zinginezo. (Maji au kidonge cha) matunda ya kranberi yanaweza kupunguza matukio katika watu wanaoambukizwa mara kwa mara. Hata hivyo, kuzoea matunda ya kranberi kwa muda mrefu ni jambo linaloweza kupelekea matatizo. Matatizoo ya tumbo na matumbo hutokea katika zaidi ya asilimia 30 ya watu wanaokunywa maji ya matunda ya kranberi au kutuia vidonge vyake.Kufikia mwaka wa 2011, probiotoki zinazotumika ndani ya uke zinzhitaji utafiti zaidi ili kutambua iwapo zina manufaa.

Matibabu kwa kutumia dawa

Kwa watu walio na maambukizi yanayojirudiarudia, matumizi ya antibiotiki kwa muda mrefu hunufaisha. Dawa zinazotumika mara nyingi ni pamoja na nitrofurantoin na trimethoprim/sulfamethoxazole. Ikiwa maambukizi yanahusiana na ngono (kujamiana), baadhi ya wanawake hunufaika kwa kutumia antibiotiki baada ya ngono. Kwa wanawake walio katika kipindi cha ukomohedhi, estrojini (aina ya homoni) ya kupakwa ukeni imetambulika kupunguza kurejea kwa maambukizi. Kinyume na malai ya kupakwa, utumizi wa estrojini ya ukeni kutokapesari haujanufaisha inapotumika kama kipimo cha kiwango cha chini cha antibiotiki. Idadi fulani ya chajo zingali zikitengenezwa kufikia mwaka wa 2011.

Katika watoto

Ushahidi kuwa antibiotiki zinazozuia hupunguza maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo katika watoto ni mdogo sana. Katika visa adimu katika watu wasio na matatizo ya figo, maambukizi yanayorejea ya mfumo wa viungo vya mkojo husababisha mataizo ya figo. Matatizo haya hupelekea chini ya theluthi ya asilimia (asilimia 0.33) ya ugonjwa wa muda mrefu wa figo katika watu wazima.

Utambuzi wa ugonjwa


Basilia (bakteria za umbo la vijiti, zilizoonyeshwa hapa kama nyeusi na za umbo la maharagwe) zilizoonyeshwa katikati ya seli nyeupe za damu zilizo kwenye sampuli ya mkojo. Mabadiliko haya yanaonyesha maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo.
Katika visa visivyo hatari, uchunguzi wa kimaabara hauhitajiki na maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo yanaweza kutambuliwa kulingana na dalili pekee. Uchanganuzi wa mkojo (kupima mkojo) unaweza kutumika kubainisha utambuzi katika matukio tata, kuchunguza uwepo wa nitraiti za mkojo chembechembe nyeupe za damu (lukosaiti) au lukosaiti esterasi. Uchuguzi mwingine, uchunguzi wa mkojo kwa kutumia hadumini, huangazia uwepo waseli nyekundu za damu, chembechembe nyeupe za damu au bakteria. uchunguzi viini wa mkojo huchukuliwa kuwa chanya iwapo utaonyesha idadi ya koloni za bakteria ikiwa 3 vitengo vinavyounda koloni 10 au zaidi kwa kila mL ya kiumbe cha kawaida cha njia ya mkojo. Uchunguzi pia unaweza kutumika kupima kiwango cha usikivu wa antibayotiki na kusaidia kubaini aina ya tiba ya antibiotiki itakayotumika. Hata hivyo, wanawake wanaotambulika kuwa na maambukizi wanaweza kuboresha afya kwa kutumia matibabu ya antibiotiki Dalili za maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo zinaweza kuwa hafifu katika watu wazee, kwa hivyo utambuzi unaweza kuwa mgumu bila kupata vipimo vya kutegemewa.

Uainishaji

Maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo yanayohusisha sehemu ya chini ya mfumo wa viungo vya mkojo hujulikana kama maambukizi ya kibofu. Maambukizi yanayohusisha sehemu ya juu ya mfumo wa viungo vya mkojo hujulikana kama pilonifritisi au maambukizi ya figo. Iwapo mkojo una bakteria nyingi lakini hakuna dalili, hali hii kujulikana kama bakteriuria. . Iwapo maambukizi yanahusisha sehemu ya juu ya mfumo wa viungo vya mkojo, mgonjwa huyu ana kisukari tamu, ana mimba, ni mume au anaudhaifu wa kingamwili (kingamwili iliyodhoofika kufuatia ugonjwa mwingine), maambukizi haya huchukuliwa kama yaliyo na matatizo.. Watoto wanapokuwa na homa pia, maambukizi haya ya mfumo wa viungo vya mkojo huchukuliwa kuwa maambukizi ya sehemu ya juu ya mfumo wa viungo vya mkojo.

                                              watoto

Ili kutambua maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo katika watoto, viini vunafaa kutambulika katika mkojo. Mara nyingi, uchafuzi husababisha changamoto hivyo kipeo cha CFU/mL 5  10 hutumika kuchukua sampuli ya kati ya "kitegeo safi", CFU/mL 4  10 hutumika kwa sampuli zilizotolewa kwa katheta, na CFU/mL 2  10 hutumika kwa mpumuo wa juu ya kinena (sampuli inayotolewa moja kwa moja kutoka ndani ya kibofu kwa kutumia sindano). The Shirika la Afya Duniani hushauri kwamba "mifuko ya mkojo" isitumiwe kuchukua sampuli kwa sababu ya kiwango cha juu cha uchafuzi wakati mkojo huo unapochunguzwa. Inapendekezwa kutumia katheta iwapo mgonjwa hawezi kutumia choo. Baadhi ya makundi ya kiafya kama vile Chuo cha Marekani cha Wanapidriatiki, hupendekeza picha za matibabu za figo na voiding sistorethrogramu ya kuvuta (kutazama urethra na kibofu cha mkojo kwa kutumia picha za moja kwa moja wanapokojoa) katika watoto wote walio na umri wa chini ya miaka 2 na wana maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo. Hata hivyo, kwa sababu kuna ukosefu wa matibabu mwafaka iwapo matatizo yatapatikana, makundi mengine kama vile Taasisi ya Kitaifa ya Fanaka ya Matibabu hushauri picha za kila mara kwa watoto wa umri wa chini ya miezi 6 au walio na matokeo ya uchunguzi yasiyo ya kawaida.

Utambuzi tofautishi

Katika wanawake walio na sevisitisi (inflamesheni ya seviksi) au vajinitisi (inflamesheni ya uke) na wavulana walio na dalili za maambukizi ya mfumo wa viungo vya mkojo, maambukizi yanaweza kuwa yamesababishwa na Chlamydia trachomatis auNeisseria gonorrheae  Vajinitisi pia inaweza kusababishwa na maambukizi ya chachu sisititisi ya ndani ya maungo (uchungu wa muda mrefu wa ndani ya kibofu) inaweza kuwa kisababishi cha dalili za mara kwa mara za maambukizi ya viungo vya mfumo wa mkojo, lakini ambao sampuli za mkojo wao havionyeshi maambukizi baada ya uchunguzi, wala hawapati nafuu baada ya kupewa antibiotiki.

Matibabu

Fenasopiridini inaweza kutumika pamoja na antibiotiki ili kupunguza muwasho wa maambukizi ya kibofu. Hata, fenasopiridini kwa sasa haitumiki kwa sababu za usalama wa kiafya, hasa hatari kuu ya methemoglobinemia (kiwango cha juu ya kawaida cha methemoglobini katika damu). Asetaminofeni inaweza kutumika kutibu homa.
Wanawake walio na maambukizi madogo na ya mara kwa mara ya viungo vya mfumo wa mkojo hunufaika kutokana na tiba ya kibinafsi; ufuatilizi wa kibinafsi utahitajika tu iwapo matibabu ya kwanza hayatafaulu. Women can ask their physicians to prescribe the antibiotics by phone




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

YOU HAVE A BRIGHT FUTURE. IF YOU WILL GIVE YOUR EARTHLY LIFE TO JESUS

https://mbochiherbal.blogspot.com But if you contract HIV you need to think through what you need to change in your life and then set to work to rebuild your immune system

WATU WA KALE WALIAMINI TANGAWIZI NI TIBA ZAIDI MAANA ILITIUBU MARADHI 28

WATU WAKALE WALITUMIA ZAO LA TANGAWIZI KAMA TIBA KWA KUTIBU TAKRIBANI MAGONJWA 28 NA 100% WALIPONA Tangawizi (kwa Kilatini zingiberis rhizoma; kwa Kiingereza: ginger) ni mzizi wa mtangawizi. Umbo la tangawizi ni kama lile la mzizi wa manjano na yote miwili hutumika kama viungo katika chakula. TANGAWIZI NI TIBA KUBWA IKITUMIWA VEMA Tangawizi huwa na utomvu wenye mafuta na kampaundi zinazofanya ukali wake. Utafiti wa kisasa umegundua tangawizi inaweza kusaidia katika matatizo ya utumbo na kuzuia kutapika Tangawizi inatazamiwa kupunguza maumivu ya viungo vilivyoathiriwa na rumatizimu na homa ya baridi yabisi (arthritis) KWENYE ELIMU YA KALE WALITUMIA TANGAWIZI KUJENGA AFYA Katika elimu ya tiba ya kale tangawizi ilitazamiwa kuwa na tabia nyingi za kujenga afya, lakini matokeo mengi yanayodaiwa mwilini hayajathibitishwa kisayansi: Imedaiwa kuwa na uwezo ufuatao wa kitiba: 1. kuondoa sumu mwilini Sumu ni dutu yoyote inayoweza kuharibu kiasi kidogo shughuli za seli au inayo...

TIBA YA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU

Shinikizo la juu la damu Shinikizo la juu la damu (HTN) au presha ya juu ya damu (pia huitwa shinikizo la mishipa ya damu , HBP), ni ugonjwa sugu ambapo nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ni kubwa kuliko kawaida. Ongezeko hilo husababisha moyo kufanya kazi kupita kiasi ili uzungushe damu katika mishipa ya damu. Kwa kawaida halina dalili, ila likidumu lina madhara makubwa kwa afya. Shinikizo la juu la damu ndilo sababu kubwa (kihatarishi) ya upoozaji, mshtuko wa moyo (mashambulizi ya moyo), moyo kushindwa kufanya kazi, kutuna kwa ukuta wa mishipa (k.m., kutuna kwa ukuta wa aota au mkole), chujio la mshipa wa kupeleka damu kwenye moyo au peripheral arterial disease, na inasababishwa na ugonjwa sugu wa figo. Hata ongezeko la wastani la shinikizo la damu hupunguza matarajio ya muda wa kuishi. Kuna vipimo viwili vya shinikizo la damu, yaani systolic na diastolic: shinikizo au presha ya systolic ni kipimo cha damu ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu katika mish...