Hatua za kuzuia kusambaza VVU kutoka kwa mama hadi mtoto zinaweza kupunguza kiwango cha maambukizi kwa asilimia 92-99. Kimsingi, hatua hizi hujumuisha kutumia mwungano wa dawa za kudhibiti VVU katika ujauzito na baada ya kuzaa, na pia kunywesha kwa chupa badala ya kunyonyesha.Ikiwa itakubaliwa kulisha, inafaidi, inawezekana kumudu gharama yake, na ni salama, kina mama hawapaswi kuwanyonyesha watoto wao. Hata hivyo, iwapo haiwezekani, kina mama hushauriwa kunyonyesha tu katika miezi ya kwanza. Ikiwa kunyonyesha pekee kutatekelezwa, kumpa mtoto proflaksisi ya kudhibiti VVU kwa muda mrefu zaidi hupunguza hatari ya kuambukizwa.
DAWA ZA KUDHIBITI VIRUSI
Kwa sasa hakuna tiba au chanjo ya VVU mwafaka. Matibabu hujumuisha dawa tendi za kudhibiti VVU za kiwango cha juu zinazopunguza mwendo wa ugonjwa huu. Kufikia mwaka 2010, zaidi ya watu milioni 6.6 wa nchi za mapato ya chini na ya kati walikuwa wakitumia dawa hizo.Matibabu pia huhusisha hatua za kuzuia na kutibu maambukizi nyemelezi.
Chaguo za kisasa za KNKN ni michanganyiko ya angalau dawa tatu za angalau aina au "vikundi" viwili vya ajenti za dawa za kudhibiti VVU. Mwanzoni, matibabu kwa kawaida huhusisha kizuizi kisicho cha nukliosidi kinachozuia kugeuzwa kwa nakala (KKNKN) pamoja na vidonge viwili vya kifanani cha nukliosidi kinachozuia kugeuzwa kwa nakala (KNKN). KNKN kwa kawaida hujumuisha: zidovudine (AZT) au tenofovir (TDF) na lamivudine (3TC) au emtricitabine (FTC).Mwungano wa ajenti zinazojumuisha kizuizi cha protisi (KP) hutumika utaratibu huu ukipoteza utendakazi
Wakati wa kuanzisha matumizi ya dawa za kudhibiti VVU ni mada ambayo ingali inajadiliwa. Shirika la Afya Duniani, miongozo ya Ulaya na pia Marekani hupendekeza dawa za kudhibiti VVU kwa vijana waliobalehe, watu wazima na kina mama wajawazito walio na kiwango cha CD4 cha chini ya 350/uL au walio na dalili, bila kuzingatia kiwango chao cha CD4.Hali hii huwezeshwa na ukweli kwamba kuanzisha matibabu wakati huu hupunguza hatari ya kifo. Isitoshe, Marekani imependekeza matibabu hayo kwa watu wote wenye VVU bila kuzingatia kiwango cha CD4 au dalili, ingawa inatoa pendekezo hili ikiwahofia watu wenye kiwango cha juu cha CD4. Shirika la Afya Duniani pia linapendekeza matibabu kwa watu wenye maambukizi nyongeza ya kifua kikuu na hepatitisi B tendi ya muda mrefu.
Matibabu yanapoanzishwa, inapendekezwa yaendelezwe bila "kupumzika".Watu wengi hutambuliwa punde tu baada ya wakati ambao matibabu yalipaswa kuanzishwa. Katika matibabu, matokeo yanayotarajiwa ni kiwango cha HIV-RNA ya plasma ya muda mrefu cha chini ya nakala 50/mL.Viwango vya kuthibitisha ikiwa matibabu ni mwafaka hupendekezwa kwanza baada ya wiki nne na punde viwango hivi vinaposhuka chini ya nakala 50/mL. Vipimo vya kila baada ya miezi 3-6 kwa kawaida huwa mwafaka. Udhibiti usio mwafaka huchukuliwa kuwa zaidi ya nakala 400/mL.Kulingana na kigezo hiki, matibabu huwa mwafaka kwa zaidi ya 95% ya watu katika mwaka wa kwanza.
Manufaa ya matibabu hujumuisha upungufu wa hatari ya kuendelezwa kwa VVU na kupunguka kwa hatari ya kifo.Katika mataifa yaliyostawi matibabu pia huboresha afya ya mwili na ya akili. Matibabu hupelekea kupunguza kwa 70% hatari ya kupata kifua kikuu. Manufaa ya nyongeza hujumuisha upungufu wa hatari ya kusambazwa kwa ugonjwa huu hadi kwa wenzi kingono, na upungufu wa kusambazwa kwa maambukizi kutoka kwa mama hadi mtoto.
Ubora wa matibabu hutegemea pakubwa maafikiano. Sababu za kutoafikiana hujumuisha: ufikiaji duni wa huduma za kimatibabu,huduma duni za kijamii, ugonjwa wa akili na uraibu wa madawa.Isitoshe, utata wa utaratibu wa matibabu (kufuatia idadi ya tembe na idadi ya marudio ya kumeza tembe) na athari kali zinaweza kusababisha kutoafikiana kwa kimakusudi.Hata hivyo, viwango vya uafikiano ni sawa katika nchi zinazostawi na zilizostawi
Matukio makuu huhusishwa na ajenti inayotumika. Baadhi ya visa vinavyotokea mara nyingi hujumuisha: sindromu ya lipodistofi, dislipidemia na kisukari tamu hasa pamoja na vizuizi vya protisi. Dalili zingine zinazotokea mara nyingi hujumuisha: kuhara, na ongezeko la hatari ya ugonjwa wa moyo na mishipa. Hata hivyo, athari kali huwa katika matibabu mapya yaliyopendekezwa. Gharama huenda ikawa tatizo kwani baadhi ya dawa huwa ghali Hata hivyo, hadi mwaka wa 2010, 47% ya watu waliohitaji dawa hizo walikuwa wakizitumia katika nchi zinazostawi na za mapato ya wastani Dawa fulani zinaweza kuhusishwa na ulemavu wa kuzaliwa hivyo hazifai kutumiwa na wanawake wanaopanga kupata watoto.
Matibabu yanayopendekezewa watoto hutofautiana kidogo na ya watu wazima. Katika nchi zinazoendelea, kufikia mwaka wa 2010, 23% ya watoto waliohitaji dawa hizi walikuwa wakizitumia. Shirika la Afya Duniani na Marekani inapendekeza matibabu kwa watoto wote wa umri wa chini ya miezi 12.Marekani hupendekeza matibabu kwa watoto wa umri wa mwaka 1-5 walio na kiwango cha VVU-RNA cha zaidi ya nakala 100,000 /mL na kwa walio zaidi ya miaka mitano watibiwe iwapo kiwango cha CD4 ni chini ya 500/ul
WASILIANA NASI;
kwa ushauri wa kiafya juu ya mama na mtoto
kwa kuepuka maambukizi nyemelezi juu ya ugonjwa wa UKIMWI
MBOCHI HERBAL LIFI MHL-HERBAL MEDICINE
- mbochiherballife646@gmail.com
- TOP 8
www.mbochiherbalife.co.tz
+255757349219/0685217438
Maoni