Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KITUNGUU SAUM UTIBU MARADHI YOTE


YAJUE VEMA MAAJABU YA KITUNGU SAUMU NA FAIDA ZAKE KATIKA KUPAMBANA NA MARADHI MWILINI
(TUMIENI SANA VITUNGUU VYA ASILI na siyo vya kisasa)



Heres Why You Should Start Your Day With Raw Garlic And Water ...


MAGONJWA YANAYOTIBIKA KUPITIA KITUNGUU SAUMU


1. Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)
2. Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I
3. Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine
4. Huzuia kuhara damu (Dysentery)
5. Huondoa Gesi tumboni
6. Hutibu msokoto wa tumbo
7. Hutibu Typhoid
8. Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi
9. Hutibu mafua na malaria
10. Hutibu kifua kikuu (ukitumia kitunguu swaumu kesho yake unaweza kutokwa na makohozi mengi tu ambayo ni ishara kwamba kweli kinatibu kifua kikuu (TB)
11. Hutibu kipindupindu
12. Hutibu upele
13. Huvunjavunja mawe katika figo
14. Hutibu mba kichwani
15 Huupa nguvu ubongo. Kazi nzuri niliyopenda zaidi katika kitunguu swaumu.
16. Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu
17. Huongeza SANA nguvu za kiume pia hutibu uanithi (kushindwa kusimama kabisa uume)
18 Hutibu maumivu ya kichwa
19 Hutibu kizunguzungu
20. Hutibu shinikizo la juu la damu
21. Huzuia saratani/kansa
22. Hutibu maumivu ya jongo/gout
23. Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
24. Huongeza hamu ya kula
25. Huzuia damu kuganda
26. Husaidia kutibu kisukari
27. Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi (ni kweli, na ni moja ya kazi nyingine ya kitunguu swaumu iliyonishangaza zaidi) pia kinaondoa msongo wa mawazo/stress na kukufanya uishi miaka mingi
28. Huongeza SANA kinga ya mwili na kwa muda mfupi, kijaribu na ulete majibu


FAIDA ZA KITUNGUU SWAUMU KATIKA MWILI WA BINADAMU

Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.

Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo hutolewa baada ya kuvila.


MADHARA YA KITUNGUU SWAUMU KATIKA MWILI WA BINADAMU


Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa, kunywa maji mengi au kutafuna karafuu. Na nimeshuhudia nikinywa kwenye mtindi hii harufu ni kama haipo kabisa na hata ukijamba haikutokei ile harufu mbaya sana kama ukinywa vitunguu swaumu katika maji

Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha. Ikikutokea kuharisha siku mbili tatu furahi kwani ni njia mojawapo ya mwili kujisafisha
Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.
Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.
Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.


NB;
kitunguu swaumu kinaweza kuwa na faida nyingi zaidi ya hizi lakini bado nakushauri utumie kiasi kidogo (punje 6 tu) kila siku kwa kipindi kirefu wiki 2 au 3 hata mwezi ili uone faida zake zaidi. Ikikutokea tangu umeanza kutumia kitunguu swaumu kichwa kinauma zaidi unaweza kupumzika siku mbili hivi na baadaye unaendelea hivyo hivyo.


Image may contain: flower







Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

YOU HAVE A BRIGHT FUTURE. IF YOU WILL GIVE YOUR EARTHLY LIFE TO JESUS

https://mbochiherbal.blogspot.com But if you contract HIV you need to think through what you need to change in your life and then set to work to rebuild your immune system

WATU WA KALE WALIAMINI TANGAWIZI NI TIBA ZAIDI MAANA ILITIUBU MARADHI 28

WATU WAKALE WALITUMIA ZAO LA TANGAWIZI KAMA TIBA KWA KUTIBU TAKRIBANI MAGONJWA 28 NA 100% WALIPONA Tangawizi (kwa Kilatini zingiberis rhizoma; kwa Kiingereza: ginger) ni mzizi wa mtangawizi. Umbo la tangawizi ni kama lile la mzizi wa manjano na yote miwili hutumika kama viungo katika chakula. TANGAWIZI NI TIBA KUBWA IKITUMIWA VEMA Tangawizi huwa na utomvu wenye mafuta na kampaundi zinazofanya ukali wake. Utafiti wa kisasa umegundua tangawizi inaweza kusaidia katika matatizo ya utumbo na kuzuia kutapika Tangawizi inatazamiwa kupunguza maumivu ya viungo vilivyoathiriwa na rumatizimu na homa ya baridi yabisi (arthritis) KWENYE ELIMU YA KALE WALITUMIA TANGAWIZI KUJENGA AFYA Katika elimu ya tiba ya kale tangawizi ilitazamiwa kuwa na tabia nyingi za kujenga afya, lakini matokeo mengi yanayodaiwa mwilini hayajathibitishwa kisayansi: Imedaiwa kuwa na uwezo ufuatao wa kitiba: 1. kuondoa sumu mwilini Sumu ni dutu yoyote inayoweza kuharibu kiasi kidogo shughuli za seli au inayo...

TIBA YA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU

Shinikizo la juu la damu Shinikizo la juu la damu (HTN) au presha ya juu ya damu (pia huitwa shinikizo la mishipa ya damu , HBP), ni ugonjwa sugu ambapo nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ni kubwa kuliko kawaida. Ongezeko hilo husababisha moyo kufanya kazi kupita kiasi ili uzungushe damu katika mishipa ya damu. Kwa kawaida halina dalili, ila likidumu lina madhara makubwa kwa afya. Shinikizo la juu la damu ndilo sababu kubwa (kihatarishi) ya upoozaji, mshtuko wa moyo (mashambulizi ya moyo), moyo kushindwa kufanya kazi, kutuna kwa ukuta wa mishipa (k.m., kutuna kwa ukuta wa aota au mkole), chujio la mshipa wa kupeleka damu kwenye moyo au peripheral arterial disease, na inasababishwa na ugonjwa sugu wa figo. Hata ongezeko la wastani la shinikizo la damu hupunguza matarajio ya muda wa kuishi. Kuna vipimo viwili vya shinikizo la damu, yaani systolic na diastolic: shinikizo au presha ya systolic ni kipimo cha damu ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu katika mish...