Ruka hadi kwenye maudhui makuu

ITAMBUE [TB] KIFUA KIKUU

ITAMBUE TB    "'KIFUA KIKUU"

M.tb resistors: M.tb uninfected or atypical IFN-𝛾-independent M ...


Kifua kikuu husambazwa kutoka kwa Mtu mmoja hadi mwingine kwa kupitia hewa wakati anapokohoa, kupiga chafya, au MATE yake yakiwa hewani

Maambukizi mengi hayana dalili wala hayaleti madhara. Lakini moja kati ya maambukizo kumi yasiyoleta madhara hatimaye huendelea na kuwa ugonjwa kamili. Kama kifua kikuu kisipotibiwa, kinaua zaidi ya 50% ya watu walioambukizwa.

Dalili za kawaida za maambukizi ya kifua kikuu kinacholeta madhara ni kikohozi sugu na kukohoa Damu, kukohoa, homa, kutokwa na jasho usiku, na kukonds. Maambukizi ya viungo vingine husababisha dalili mbalimbali. Njia ya kitaalamu ya utambuzi wa kifua kikuu kwa kutumia  Eksirei ya kuchunguza ugonjwa hujulikana kama eksirei ya kifua na pia wanatumia hadubini na kufanya uchunguzi wa vimelea maradhi vya majmaji ya mwilini. Uchunguzi wa kifua kikuu kisicholeta madhara hutumia kipimo kiitwachokipimo cha ngozi (TST) na vipimo vya damu.

TIBA si rahisi na inabidi kupewa dawa nyingi za kinga mwili kwa kipindi kirefu. Mawasiliano ya kijamii pia yanapimwa na kutibiwa kama inavyotakiwa. Dawa zinzzoshindwa kutibu magonjwa ni tatizo kubwa la maambukizi sugu mengi ya kifua kikuu


KIFAHAMU KIFUA KIKUU [TB]


Kifua Kikuu (Tuberculosis) ni ugonjwa wa kuambukiza ambao mara nyingi hushambulia mapafu. Ugonjwa huu unachukua nafasi ya pili duniani ya vifo vinavyotokana na maambukizi yanayotokana na kitu kimoja.

Katika mwaka 2015 peke yake, watu wapatao milioni 1.8 walikufa kwa ugonjwa huu kutoka idadi ya watu milioni 10.4 waliougua kifua kikuu.


Katika miaka ya katikati ya karne za 18 na 19, kulitokea milipuko ya ugonjwa huu huko Ulaya na Marekani Ya Kaskazini, kabla ya mwanasayansi kutoka Ujerumani, Robert Koch, kumgundua bakteria anayesababisha kifua kikuu mwaka 1882.

Kufuatia ugunduzi wa Robert Koch, ugunduzi na utumiaji wa chanjo na dawa za kuponya kifua kikuu ulileta imani kuwa ugonjwa huu ungetokomezwa. Mara moja Shirika la Umoja Wa Mataifa lilibashiri kuwa ugonjwa huu utakuwa umetokomezwa kufikia 2025.

Lakini katika miaka ya kati ya 1980 na 1990, TB iliongezeka kwa kasi duniani, hivi kwamba mwaka 1993 Shirika La Afya Duniani (WHO) lilitangaza hali ya hatari, kwa mara ya kwanza kabisa ugonjwa kutangazwa kwa namna hiyo.

Kwa bahati nzuri, kwa kufuata tiba kikamilifu, watu wengi waliopata TB hupona. Bila kupewa tiba nzuri, katika idadi ya wagonjwa wote wa TB, wagonjwa wafikiao hadi theluthi mbili watafariki dunia.

 

Tuberculosis Ni Nini?

 

Madakatari hutofautisha kati ya aina mbili za maambukizi ya kifua kikuu: latent na active.

 

Tuberculosis management - Wikipedia

 

Latent TB – bakteria hubaki ndani ya mwili bila kuleta madhara. Hawatoi dalli zo zote, na hawaambukizi, lakini wanaweza kuja kuanza kuleta madhara.

Active TB – bakteria wanaleta madhara na wanaweza kuambukiza kwa wengine.

Inaaminika kuwa karibu theluthi moja watu duniani wana latent TB. Kuna asilimia 10 ya uwezekano wa watu hawa kupata active TB, uwezekano huo ukichagizwa na upungufu wa kinga za mwili au kukosa mlo wa kutosha au kuvuta sigara.

TB ni ugonjwa unaoshambulia watu wa rika zote na watu wa pande zote za dunia. Lakini ugonjwa huu hushambulia vijana na watu wanaoishi kwenye nchi zinazoendelea. Takwimu za 2012 zilionyesha kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wa TB walitoka katika nchi 22 tu.

 

Kifua Kikuu Husababishwa Na Nini?




World Tuberculosis Day 2020: TB Symptoms, Risk Factors, and Prevention




 

TB husababishwa na bakteria aitwaye Mycobacterium tuberculosis. Bakteria huyu husambaa kwenye hewa wakati mtu mwenye TB (ambaye mapafu yake yameshambuliwa) akikohoa, akipiga chafya,akitema mate, akicheka , au akizungumza.

TB huambukizwa lakini siyo rahisi kuipata. Uwezekano wa kupata TB kutoka kwa mtu unayeishi au kufanya kazi naye ni mkubwa kuliko kutoka kwa mgeni. Watu wengi ambao tayari wamaeanza tiba sahihi angalau kwa wiki 2 hawaambukizi.

Toka antibiotics zilipoanza kutumika kutibu TB, baadhi ya aina ya bakteria hao wamegeuka sugu kwa dawa. Multidrug-resistant TB (MDR-TB) ni hali ambapo dawa haziwezi tena kuwaua bakteria wote, bakteria wanaosalia wakijijengea usugu wa dawa hiyo na dawa nyngine pia kwa wakati mmoja.

Multidrug-resistant TB (MDR-TB) inatibika kwa kutumia dawa za kipekee (very specific anti-TB drugs) ambazo ni chache na hazipatikani kirahisi. Katika mwaka 2012, karibu watu 450,000 walipata MDR-TB.

Watu wenye upungufu wa kinga za mwili huwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata active TB. HIV Udhoofisha kinga za mwili, na kuufanya mwili kupata shida ya kudhibiti bakteria wa TB. Watu wenye mchanganyiko wa HIV na TB wana uwezekano wa kupata active TB kwa kiwango cha ailimia 20-30 ukilinganisha na wale ambao hawana HIV.

Matumizi ya tumbaku yamedhirika kuongeza uwezekano wa kupata active TB. Aslimia 20 ya TB duniani huhusishwa na matumizi ya tumbaku.

 

Dalili Za Kifua Kikuu

 

Wakati latent TB haina dalili zozote, active TB huwa na dalili zifuatazo:

. Kukohoa, wakati mwingine kukiwa na makohozi au damu
. Kusikia baridi
. Uchovu
. Homa
. Kukonda kwa mwili
. Kukosa hamu ya kula
. Kutoa jasho usiku

 

dalili za kifua kikuu

 

Kifua kikuu huathiri hasa mapafu, lakini kinaweza kuathiri vile vile sehemu nyingine za mwili. Wakati TB imeathiri sehemu tofauti ya mwili, dalili zinaweza kubadilika. Bila kupata tiba, TB huweza kusambaa kwenye sehemu nyingine za mwili kupitia mfumo wa damu.

. Tb ikishambulia mifupa inaweza kuleta maumivu ya uti wa mgongo na kuharibu maungio ya mifupa
. TB ikishambulia ubongo husababisha meningitis
. TB ikishambulia maini na figo huweza kusababisha damu ndani ya mkojo
. TB ikishambulia moyo inaweza kuathiri uwezo wa moyo wa kusukuma damu na kusababisha cardiac tamponade ambayo inaweza kuua.

 

Tiba Ya Kifua Kikuu

 

Wagonjwa wengi wa TB wanaweza kupona kama dawa stahiki itakuwepo na kutolewa inavyopaswa. Aina ya dawa na urefu wa muda wa matumizi vitategemea umri wa mgonjwa, hali yake ya afya kwa ujumla, usugu wa mwili wake kwa dawa, kama TB in latent au active, sehemu yake ya mwili iliyoathirika (i.e mapafu, ubongo, figo)
Watu wenye latent TB wanaweza kuhitaji aina moja tu ya dawa, wakati watu wenye active TB (na hasa MDR-TB) watahitaji mchanganyiko wa dawa.

 

How to treat tuberculosis naturally! | Looven

 

Antibiotics za TB hutakiwa kutumiwa kwa muda mrefu kidogo, muda wa wastani ukiwa ni miezi 6.

Matumizi ya dawa za kifua kikuu huweza kusababisha sumu kwa ini, ingawa ni mara chache hili kutokea, linapotokea, linaweza kuleta matatizo makubwa. Madhara ya dawa hizi yanapojitokeza, ni lazima taarifa itolewe kwa daktari. Madhara hayo ni pamoja na:
.  Mkojo mweusi
.  Homa
.  Homa ya manjano
.  Kukosa hamu ya kula
.  Kichefuchefu na kutapika

Ni muhimu kwa mgonjwa kuhakikisha kuwa anamaliza dawa, hata kama dalili za TB zitakuwa zimeondoka. Bakteria waliosalia na kuvumilia tiba iliyotolewa wanaweza kugeuka sugu kwa tiba hiyo na kupelekea kupata MDR-TB hapo baadaye.

Kataka mada nyingine tatajadili kuhusu UGONJWA wa homa ya Ini [Haepatitis]

Ndugu msomaji, usisite kutoa maoni yako au kuuliza maswali kuhusu mada hii. Tutafurahi kuwa nawe na kukujibu.

 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

VIAGRA YA ASILI

  Pata Kijiko zaidi katika malisho yako. MTINDO WA MAISHA Vyakula 10 ambavyo vinaweza kutenda kama Viagra asili Ikiwa unakuwa na shida chumbani, au unatafuta tu viungo, vyakula hivi hufanya kazi kama aphrodisiac na kuchukua nafasi ya hitaji la Viagra - ambayo, kwa matumaini, hautalazimika kutumia kwa muda .  Ongeza hizi wakati wa chakula cha jioni, na itahakikisha kuwa vitu vinakaa vya kupendeza ukimaliza dessert na bado unatamani kitu kitamu .. Hatukulaumu pia ikiwa unataka kula vyakula hivi kwa kuzimu tu, kwa sababu mara nyingi, chakula ni   bora zaidi kuliko ngono  . 1. Celery Picha na Herbalist Thobias Beda Celery inaweza kuonja kama maji na kuwa nyembamba sana, lakini ina arginine, ambayo  hupanua mishipa ya damu  kwa njia sawa na Viagra.  Pia ina steroids mbili ambazo husaidia kuboresha harufu ya mwili wetu, na kutufanya tuvutie wengine.  Chop mabua machache na uyatie kwenye  hummus hii  . 2. Tikiti maji Picha na Herbalist Tho...

YOU HAVE A BRIGHT FUTURE. IF YOU WILL GIVE YOUR EARTHLY LIFE TO JESUS

https://mbochiherbal.blogspot.com But if you contract HIV you need to think through what you need to change in your life and then set to work to rebuild your immune system

WATU WA KALE WALIAMINI TANGAWIZI NI TIBA ZAIDI MAANA ILITIUBU MARADHI 28

WATU WAKALE WALITUMIA ZAO LA TANGAWIZI KAMA TIBA KWA KUTIBU TAKRIBANI MAGONJWA 28 NA 100% WALIPONA Tangawizi (kwa Kilatini zingiberis rhizoma; kwa Kiingereza: ginger) ni mzizi wa mtangawizi. Umbo la tangawizi ni kama lile la mzizi wa manjano na yote miwili hutumika kama viungo katika chakula. TANGAWIZI NI TIBA KUBWA IKITUMIWA VEMA Tangawizi huwa na utomvu wenye mafuta na kampaundi zinazofanya ukali wake. Utafiti wa kisasa umegundua tangawizi inaweza kusaidia katika matatizo ya utumbo na kuzuia kutapika Tangawizi inatazamiwa kupunguza maumivu ya viungo vilivyoathiriwa na rumatizimu na homa ya baridi yabisi (arthritis) KWENYE ELIMU YA KALE WALITUMIA TANGAWIZI KUJENGA AFYA Katika elimu ya tiba ya kale tangawizi ilitazamiwa kuwa na tabia nyingi za kujenga afya, lakini matokeo mengi yanayodaiwa mwilini hayajathibitishwa kisayansi: Imedaiwa kuwa na uwezo ufuatao wa kitiba: 1. kuondoa sumu mwilini Sumu ni dutu yoyote inayoweza kuharibu kiasi kidogo shughuli za seli au inayo...