Ruka hadi kwenye maudhui makuu

VIDONDA VYA TUMBO;- CHANZO & TIBA YAKE YA KIASILI



































































































                           UJUE UGONJWA WA VIDONDA VYA TUMBO




Tiba na dalili za vidonda vya tumbo na 12 duodenal ulcer


Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda, hii hutokea ni baada ya kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaoitwa mucus. Kemikali ambayo ni acidi inayozalishwa mwilini kiasili husaidia kuyeyusha chakula na kuua wadudu tumboni, kama ukuta wenye ute ukiharibiwa na kushindwa kufanya kazi basi kemikali (acid) itaathiri tumbo au utumbo na kuruhusu bakteria kuendelea kusababisha vidonda vya tumbo.

Vidonda vya tumbo vinatibika kirahisi ila vikicheleweshwa bila kutibiwa huweza kusababisha tatizo kubwa. Ni tatizo linalotesa sana na kuwanyima raha watu wengi, linahitaji umakini na pia husababisha magonjwa mengine kama kansa, amoeba (amiba), homa, kupungua uzito.

 AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO


Kuna aina zipatazo mbili za Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers)

  1. Vidonda vya tumbo kubwa (Gastric ulcers) – Hivi ni vidonda vya tumbo vinavyotokea ndani kwenye tumbo kubwa

Gastric_Ulcer-1200x720

2. Vidonda vya utumbo mdogo (Duodenal ulcers) – Hivi ni vidonda ambavyo hutokea kwenye utumbo mdogo (hasa juu)

duodenal-ulcer

CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO


Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ili vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni;

  1. Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori)
  2. Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine)
  3. Kuwa na mawazo mengi
  4. Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi
  5. Kunywa pombe na vinywaji vikali
  6. Uvutaji wa sigara
  7. Kuto kula mlo kwa mpangilio

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO


Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na endelea kukuza tatizo, vidonda vya tumbo vinadalili kama;

gastrita

  1. Kupata maumivu ya tumbo yanayokuwa kama ya moto (kuunguza) baada na kabla ya kula
  2. Kupatwa na kiungulia karibu na chembe ya moyo
  3. Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa
  4. Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu
  5. Kupata haja kubwa ya rangi kahawia au nyeusi yenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu
  6. Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
  7. Kushindwa kupumua vizuri

JINSI YA KUEPUKANA NA VIDONDA VYA TUMBO


  1. Kunywa maji mengi
  2. Punguza mawazo, fanya mazoezi yatakupunguza na mawazo
  3. Punguza (balansi) kiwango cha halemu (choresterol)
  4. Usivute sigara
  5. Punguza au acha kunywa pombe
  6. Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali
  7. Lala vizuri kwa muda mzuri – masaa 7 hadi 9

TIBA YA VIDONDA VYA TUMBO


Tatizo la Vidonda vya tumbo linatibika kufuatana na mda wa tatizo, mara nyingi wagonjwa wamekuwa wakizalau dalili za vidonda vya tumbo na kudhani kuwa hakuna madhara makubwa.


DAWA YA VIDONDA VYA TUMBO


Tuna dawa ya kutibu Vidonda vya tumbo ambayo ni ya asili isiyo na kemikali ambayo hufanya mtu kupona na kuimarika kabisa. Dawa hiyo hutibu kwa mda kulingana na mda wa tatizo, tatizo halirudi tena maana huondoa chanzo pamoja na ugonjwa sio kituliza maumivu,  ukianza kutumia baada ya wiki moja mgonjwa huanza kupona na huonesha mabadiliko, pia mgonjwa anapewa mfumo wa maisha ambao inatakiwa autumie kwasababu kuna mtindo wa maisha unaendelea kuongeza tatizo pia kuna mtindo unapunguza hatari ya ugonjwa.

Tunamshukru Mungu kwa uumbaji wake na kutupa dawa ambazo alizileta ili kutuimarisha na kutuponya, Mungu hakuumba dawa nyingine zaidi ya mimea na vitu vingine vya asili, japo wengi hudharau. Mungu tunaomba utuokoe na kutuponya.


 

MAWASILIANO

mbochi herbal life

BARUA pepe;

mbochiherballife646@gmail.com

Mob; +255757349219

WE TREAT BUT GOD CURE

Vyakula tiba kwa wagonjwa wa vidonda vya tumbo - Global Publishers

MBOCHI HERBAL LIFE tuna kujali na kukupenda hivyo tuna kuandaa kiafya na kuipigania yako hali upate kutengemaa upate kuwa na afya njema TUNA KUPENDA amini ukitumia dawa yetu umepona maana MWENYEZI MUNGU katupa maarifa ya kupata dawa lakini anae tibu ni yeye




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

YOU HAVE A BRIGHT FUTURE. IF YOU WILL GIVE YOUR EARTHLY LIFE TO JESUS

https://mbochiherbal.blogspot.com But if you contract HIV you need to think through what you need to change in your life and then set to work to rebuild your immune system

WATU WA KALE WALIAMINI TANGAWIZI NI TIBA ZAIDI MAANA ILITIUBU MARADHI 28

WATU WAKALE WALITUMIA ZAO LA TANGAWIZI KAMA TIBA KWA KUTIBU TAKRIBANI MAGONJWA 28 NA 100% WALIPONA Tangawizi (kwa Kilatini zingiberis rhizoma; kwa Kiingereza: ginger) ni mzizi wa mtangawizi. Umbo la tangawizi ni kama lile la mzizi wa manjano na yote miwili hutumika kama viungo katika chakula. TANGAWIZI NI TIBA KUBWA IKITUMIWA VEMA Tangawizi huwa na utomvu wenye mafuta na kampaundi zinazofanya ukali wake. Utafiti wa kisasa umegundua tangawizi inaweza kusaidia katika matatizo ya utumbo na kuzuia kutapika Tangawizi inatazamiwa kupunguza maumivu ya viungo vilivyoathiriwa na rumatizimu na homa ya baridi yabisi (arthritis) KWENYE ELIMU YA KALE WALITUMIA TANGAWIZI KUJENGA AFYA Katika elimu ya tiba ya kale tangawizi ilitazamiwa kuwa na tabia nyingi za kujenga afya, lakini matokeo mengi yanayodaiwa mwilini hayajathibitishwa kisayansi: Imedaiwa kuwa na uwezo ufuatao wa kitiba: 1. kuondoa sumu mwilini Sumu ni dutu yoyote inayoweza kuharibu kiasi kidogo shughuli za seli au inayo...

TIBA YA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU

Shinikizo la juu la damu Shinikizo la juu la damu (HTN) au presha ya juu ya damu (pia huitwa shinikizo la mishipa ya damu , HBP), ni ugonjwa sugu ambapo nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ni kubwa kuliko kawaida. Ongezeko hilo husababisha moyo kufanya kazi kupita kiasi ili uzungushe damu katika mishipa ya damu. Kwa kawaida halina dalili, ila likidumu lina madhara makubwa kwa afya. Shinikizo la juu la damu ndilo sababu kubwa (kihatarishi) ya upoozaji, mshtuko wa moyo (mashambulizi ya moyo), moyo kushindwa kufanya kazi, kutuna kwa ukuta wa mishipa (k.m., kutuna kwa ukuta wa aota au mkole), chujio la mshipa wa kupeleka damu kwenye moyo au peripheral arterial disease, na inasababishwa na ugonjwa sugu wa figo. Hata ongezeko la wastani la shinikizo la damu hupunguza matarajio ya muda wa kuishi. Kuna vipimo viwili vya shinikizo la damu, yaani systolic na diastolic: shinikizo au presha ya systolic ni kipimo cha damu ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu katika mish...