Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TATIZO LA UKE KUTOA ARUFU MBAYA

TATIZO LA UKE KUTOA ARUFU MBAYA

Top 9 Causes Of Vaginal Odor - The Complete Herbal Guide

Wapendwa leo najibu swali la mpendwa @.... miongoni mwa wanao soma makala za MBOCHI HERBAL LIFE-24
AKIULIZA JE? NI  kwa nini uke unatoa arufu mbaya wakati wa kushiriki Tendo la kujamiana Na hii utokea pale tu unapo furaiya uumbaji ndipo panatoa arufu chafu

Leo ningependa tuzungumzie tatizo la uke kutoa harufu mbaya, kwani ni tatizo ambalo linawaathiri dada zetu sana, na huwafanya wasiwe na uhuru wanapokuwa faragha na wapenzi wao, na kuwafanya wasiwe na raha, na kupoteza kujiamini.
Tatizo la kutoa harufu ukeni husababishwa na sababu kadhaa Kama ifuatavyo.

1.Bacterial vaginosis



What To Know About Bacterial Vaginosis: Garden OB/GYN: Obstetrics


Kwa kawaida, uke huwa na bakteria ambao huitwa lactobacilli, bakteria hawa ni wazuri na hawamletei shida yeyote mwanamke, bakteria hawa huulinda uke usishambuliwe na bakteria wabaya ambao ndio husababisha magonjwa. Kinachowawezesha bakteria hawa waweze kukaa kwenye uke ni hali ya utindikali wa uke(vaginal acidity); hali hii ya utindikali wa uke inapobadilika na kupungua kwa sababu yeyote ile, husababisha bakteria hawa kupungua, na hivyo kutoa nafasi kwa bakteria wabaya kukua kwa wingi, na kushambulia afya ya uke, hivyo kusababisha harufu(harufu hii hutokana na uchafu unaotengenezwa na bakteria hawa).Hali hii kitaalamu ndio huitwa bacterial vaginosis.Ni muhimu kufahamu kuwa ugonjwa huu hauambukizwi kwa njia ya zinaa, japokuwa wanawake ambao wanajihusisha katika ngono wanakuwa katika hatari kubwa zaidi ya kpata ugonjwa huu, pia wanwake wanaofanya “douching”(kujisafisha ukeni kwa kuingiza kidole) na wanaoshiriki mapenzi kinyume cha maumbile wako kwenye uwezekano mkubwa wa kupata bacterial vaginosis.


2.Magonjwa ya zinaa (Sexually transmitted diseases;Vaginal Trichomoniasis, gonorrhea,chlamydia)



Fun With Microbiology (What's Buggin' You?): Trichomonas vaginalis


Ugonjwa wa zinaa unaoitwa kitaalamu vaginal trichomoniasis ndio ugonjwa wa zinaa ambao unaathiri wanawake wengi zaidi kuliko ugonjwa mwingine wowote wa zinaa. Ugonjwa huu unasababishwa na protozoa anaejulikana kwa jina la Trichomona vaginalis. Na huambukizwa kwa njia ya ngono. Dalili za ugonjwa huu kwa wanawake ni kutoa majimaji yanayotoa harufu kali, yenye rangi ya njano–kijani,kuwashwa ukeni.
Gonorrrhea kwa kawaida pia huweza kusababisha kutokwa na majimaji yenye harufu ukeni, na kuwashwa, maumivu wakati wa kukojoa, maumivu wakati wa kufanya mapenzi, na maumivu chini ya kitovu (japokuwa, kwa gonorhea wanawake wengi wanaweza wasionyeshe dalili yoyote kwa muda mrefu).
Mara nyingi, inaweza kuwa vigumu kwa daktari kuweza kutofautisha baina ya magonjwa haya ya zinaa (hasa kwa mazingira yetu duni); Hivyo basi mara nyingi daktari atatoa dawa kwa ajili ya magonjwa haya matatu ya zinaa pale anapofikiri kuwa mgonjwa wake ana tatizo la ugonjwa wa zinaa.


3.Fangasi za ukeni (Vagina candidiasis)



Definition of Vaginal yeast infection - All Art Online



Fangasi za ukeni pia huweza kusababisha kutokwa na harufu kali ukeni, japokuwa si kwa kiwango kikubwa sana kama sababu mbili hapo juu. Pia, mara nyingi mwanamke mwenye tatizo la fangasi za ukeni atalalamika kuhusu kuwashwa zaidi kuliko harufu.
Dalili za fangasi za ukeni ni pamoja na kutoa majimaji mazito ya rangi nyeupe (kama maziwa mtindi) yenye harufu, kuwashwa ukeni,pamoja na kusikia maumivu wakati wa kufanya mapenzi.
Vitu ambavyo vinamuweka mwanamke katika hatari ya kupata fangasi za ukeni ni pamoja na kufanya “douching” (kujisafisha uke kwa kuingiza kidole), kuvaa nguo za kubana, kuvaa nguo za ndani ambazo sio za cotton, kuvaa nguo za ndani ambazo hazijapigwa na jua/kupigwa pasi, usafi hafifu wa sehemu za siri, matumizi ya vyoo vya kukaa na matumizi ya dawa za uzazi wa mpango.


Je, nini cha kufanya ili kujiepusha na harufu mbaya ya sehemu za siri kwa mdada?


-Epuka kusafisha uke kwa kuingiza kidole ukeni-Uke usafishwe kwa maji ya vuguvugu na sabuni ya kawaida ya kuogea (sio medicated soap), bila kuingiza kidole au kitu chochote ndani ya uke
-Epuka matumizi ya madawa ya antibiotics kwa muda mrefu bila ya kuambiwa na daktari-kwani dawa hizi zikitumika kwa muda mrefu na bila ushauri wa daktari husababisha mabadiliko katika bakteria wa kwenye uke na kupelekea magonjwa na harufu mbaya

-Vaa nguo za ndani za cotton
-Epuka nguo za kubana sana mwili
-Nguo ya ndani ianikwe nje; sehemu ambayo itapigwa na jua (na sio ndani ya chumba); au nguo za ndani zipigwe pasi kabla ya kuvaliwa,
-Unapokuwa kwenye siku zako zingatia usafi na kubadilisha pedi kama inavyotakiwa(mara 2-3 kwa siku)
-Epuka kutumia vyoo vya umma ambavyo ni vya kukaa,
-Jikinge na magonjwa ya zinaa,
-Epuka kuvaa nguo nyingi na/au nzito wakati wa kulala; vaa nguo nyepesi ambayo itaruhusu uke kupata hewa ya kutosha.
-Jisafishe vizuri kila baada ya kumaliza haja ndogo,
-Kitu kingine ambacho ni muhimu sana kufahamu, ikitokea ukaona kuwa uke wako unatoa harufu, kuuosha kwa maji mengi na sabuni nyingi mara nyingi, sio suluhisho bali unazidi kuleta matatizo zaidi kwa sababu unazidi kupunguza idadi ya bakteria wazuri, na kubadilisha hali ya utindikali wa uke na hivyo kukaribisha bakteria wabaya kwa wingi zaidi!!
-Na kitu cha mwisho ambacho ni muhimu zaidi, ni kwetu wanaume, unapoona mwenzi wako ana tatizo hili, usimseme vibaya au kumkaripia au kumtukana; Unatakiwa kutambua kuwa huo ni ugonjwa na umsaidie kuweza kuonana na wataalamu wa tiba kwa ajili ya matibabu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

YOU HAVE A BRIGHT FUTURE. IF YOU WILL GIVE YOUR EARTHLY LIFE TO JESUS

https://mbochiherbal.blogspot.com But if you contract HIV you need to think through what you need to change in your life and then set to work to rebuild your immune system

WATU WA KALE WALIAMINI TANGAWIZI NI TIBA ZAIDI MAANA ILITIUBU MARADHI 28

WATU WAKALE WALITUMIA ZAO LA TANGAWIZI KAMA TIBA KWA KUTIBU TAKRIBANI MAGONJWA 28 NA 100% WALIPONA Tangawizi (kwa Kilatini zingiberis rhizoma; kwa Kiingereza: ginger) ni mzizi wa mtangawizi. Umbo la tangawizi ni kama lile la mzizi wa manjano na yote miwili hutumika kama viungo katika chakula. TANGAWIZI NI TIBA KUBWA IKITUMIWA VEMA Tangawizi huwa na utomvu wenye mafuta na kampaundi zinazofanya ukali wake. Utafiti wa kisasa umegundua tangawizi inaweza kusaidia katika matatizo ya utumbo na kuzuia kutapika Tangawizi inatazamiwa kupunguza maumivu ya viungo vilivyoathiriwa na rumatizimu na homa ya baridi yabisi (arthritis) KWENYE ELIMU YA KALE WALITUMIA TANGAWIZI KUJENGA AFYA Katika elimu ya tiba ya kale tangawizi ilitazamiwa kuwa na tabia nyingi za kujenga afya, lakini matokeo mengi yanayodaiwa mwilini hayajathibitishwa kisayansi: Imedaiwa kuwa na uwezo ufuatao wa kitiba: 1. kuondoa sumu mwilini Sumu ni dutu yoyote inayoweza kuharibu kiasi kidogo shughuli za seli au inayo...

TIBA YA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU

Shinikizo la juu la damu Shinikizo la juu la damu (HTN) au presha ya juu ya damu (pia huitwa shinikizo la mishipa ya damu , HBP), ni ugonjwa sugu ambapo nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ni kubwa kuliko kawaida. Ongezeko hilo husababisha moyo kufanya kazi kupita kiasi ili uzungushe damu katika mishipa ya damu. Kwa kawaida halina dalili, ila likidumu lina madhara makubwa kwa afya. Shinikizo la juu la damu ndilo sababu kubwa (kihatarishi) ya upoozaji, mshtuko wa moyo (mashambulizi ya moyo), moyo kushindwa kufanya kazi, kutuna kwa ukuta wa mishipa (k.m., kutuna kwa ukuta wa aota au mkole), chujio la mshipa wa kupeleka damu kwenye moyo au peripheral arterial disease, na inasababishwa na ugonjwa sugu wa figo. Hata ongezeko la wastani la shinikizo la damu hupunguza matarajio ya muda wa kuishi. Kuna vipimo viwili vya shinikizo la damu, yaani systolic na diastolic: shinikizo au presha ya systolic ni kipimo cha damu ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu katika mish...