Ruka hadi kwenye maudhui makuu

HII NDIYO TIBA YA PID [PELVIC INFLAMMATORY DISEASE]



UGONGWA WA PID PELVIC INFLAMMATORY DISEASE UNATOKANA NA NINI





SWALI PID NI NINI?


What Is PID? Treatment, Diagnosis, Causes & Pictures


Maambukizi kwenye njia ya uzazi au kwa kifupi PID, ni mambukizi ya bacteria yanayoathiri sana wanawake kwenye mfumo wa uzazi. Na kuweza kuleta athari katika sehemu zozote kwenye njia ya uzazi.moja ya athari za PID  ambayo wanawake hupata ni kutoweza kushika mimba yaani ugumba. Tafiti zinasema kati ya wanawake nane walaiowahi kuugua PID basi mmoja wao atakutana na shida kupata mimba kwa siku za hapo baadae huku wale wanaofanikiwa kupata ujauzito basi hupata matatizo pia ikiwemo mimba kuharibika au kujifungua kabla ya wakati.

Nini kinasababisha PID?? Wataalamu wa afya wanaamini kwamba magonjwa ya zinaa ambayo hayakutibiwa ipasavyo hasahasa gonorrhea na chlamydia yanaongoza kwa kusababisha PID, japo kuna baadhi ya wanawake wanaugua PID kuna kwenye maambukizi ya kawaida ya bacteria(bacteria vagonosis)

Nini Maana Ya Pelvic Inflammatory Disease(PID)

Pelvic Inflammatory Disease Stock Illustrations - Getty Images

Maana halisi ya PID ni hali ya kututumka au kucharuka kwa sehemu ya njia ya uzazi kwa mwanamke, sehemu hizi ni kama mirija ya uzazi au ovary ambako kunasababishwa na magonjwa yanayosambazwa kwa njia ya ngono.

Maambukizi kwenye njia ya uzazi (PID) yana tabia ya kusambaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na ndio maana kuna umuhimu wa kutibu tatizo hili mapema. Maambukizi haya yanaweza kusambaa kutoka kwenye uke mpaka sehemu zingine za uzazi wa mwanamke kama mirija ya uzazi, mifuko ya mayai(ovari) na kwenye shingo ya kizazi(cervix). Maambikizi haya yanaweza kusababisha makovu kwenye mirija ya uzazi na kupelekea kupata Ectopic pregnancy ambayo ni mimba iliyotungwa na kushindwa kusafiri kuelekea kwenye mfuko wa mimba(uterus) kutokana na majeraha kwenye mirija.

Dalili Za Pelvic Inflammatory Disease(PID)

Dalili za PID zinatofautiana kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kwa baadhi ya wanawake dalili huwa mbaya na kwa wengine dalili huwa za kawaida, wakati mwingine wanawake hukaa na ugonjwa kwa muda mrefu bila kujua kutokana na kuchanganya dalili na magonjwa mengine.zifuatazo ni dalili zinazojotokeza zaidi kwa wanawake wengi

  • Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ambayo yanaweza kuwa upande mmmoja au pande zote kulia na kushoto
  • Sehemu za uke kuwa na ulaini sana
  • Kupata maumivu wakati watendo la ndoa wakati mwingine kupeleekea kuvuja damu wakati na baada ya tendo la ngono na hivo kukosa tena hamu ya TENDO LA NDOA
  • Kuvurugika kwa hedhi
  • Kutokwa na majimaji ukeni kusiko kawaida hasa yenye rangi ya njano na kijani
  • Maumivu wakati wa kukojoa
  • Kupata maumivu wakati wa choo
  • Kupata dalili za homa kama kizunguzungu, mwili kukosa nguvu, kukosa hamu ya kula na uchovu mwingi.

Madhara Yanayosababishwa Na Maambukizi Kwenye Njia Ya Uzazi  (PID)

Maambukizi kwenye njia ya uzazi husababisha athari kubwa sana kwa mwanamke,kama tulivoona pale juu PID inaweza kusababisha UGUMBA na mimba kujishikiza mahali pasipo sahihi(ectopic pregnancy) tofauti na mfuko wa mimba. Kadiri unavoumwa zaidi PID ndivyo hatari ya kupata ugumba inavoongezeka. Mimba kutokea nje ya mfuko wa mimba ni ishu kubwa ya kiafya na inahitaji uangalizi mkubwa wa kidactari ili kuzuia kuvuja kwa damu na hatimae kupelekea kifo kwa mama. Madhara mengine ya PID ni

  • Kupata majeraha kwenye mirija ya uzazi, majeraha yanaweza kutokea nje ama ndani, tatizo hili linaweza kuwa gumu kutibika na hutokea tu pale ambapo maambukizi hayakutibiwa kwa muda mrefu zaidi.
  • Kuziba na KUJA MAJI KWA MIRIJA YA UZAZI [Hydrosalpinx] kutokana na majeraha ya tishu zake
  • Maumivu ya tumbo ya muda mrefu husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa na mwanamke kutofurahisa unyumba.
  • Kuongezeka kwa hatari ya kupata matatizo mengine wakati wa ujauzito na kujifungua.

Kama tulivokwisha kusoma kwamba PID huletekezwa kwa kiasi kikubwa na magonjwa ya zinaa ambayo hayakutibiwa vizuri (sexual transmitted diseases). Kwa hivo basi ni muhimu kufahamu dalili za magonjwa ya zinaa ambayo ni common sana kwenye jamii yetu kama GONORRHEA [Kisonono] na chlamydia. Ugonjwa wa Chylamidia ni ugonjwa wa zinaa unaowaathiri wake kwa wanaume na husambazwa kupitia uke, njia ya haja kubwa na pia ngono ya mdomo.

Magonjwa haya ya ngono ambayo yanasababisha PID huwa na dalili karibu sawa kwa kila mwanamke

  • Kutokwa na uchafu kupita kiasi wenye rangi ya njano na kijanina unaonuka kwenye uke
  • Kupata maumivu makali wakati wa kukojoa na kutoa haja kubwa
  • Kutokwa na uchafu mweupe kwenye uume unaoambatana na maumivu makali
  • Maumivu na kuvimba kwa kende/mapumbu
  • Kwa baadhi ya watu hupata maumivu mahala pa haja kubwa na kutokwa na uchafu

Ugonjwa Wa PID Husababishwa Na Nini? Je Zipi ni tiba sahii

Kwa kiasi kikubwa wanawake waliopo chini ya umri wa miaka 35 wanaathirika zaidi na maambukizi kwenye njia za uzazi, kutokana na kwamba wanajihusisha zaidi na ngono. Tumeona hapo juu kwamba kutokutibiwa vyema kwa maradhi ya gonorrhea na chlamydia ndio chanzo kikubwa cha PID, achilia mbali sababu hii, baadhi ya bacteria wengine wanaweza pia kusababisha PID, bacteria wengine wanaweza kuambukizwa wakati wa tendo la ngono, au wakati wa kujifungua, au kwenye kitendo cha utoaji mimba na kisha wakajificha kwenye njia ya uzazi wakaanza kukua taratibu na kusambaa.baadhi ya bacteria ambao wamegundulia kusababisha PID ni hawa wafuatao

  • Chlamydia trachomatis
  • Neisseria gonorrheae
  • Mycoplasma genitalium

Sababu Hatarishi Zinazo Ongeza Uwezekano Wa Kupata Maambukizi Kwenye Njia Ya Uzazi
  • Kundi la wanawake wenye umri kati ya miaka 25 mpaka 35
  • Kufanya ngono bila kinga
  • Wanawake waliowahi kuugua PID huko nyuma ama kupata maambukizi mengine ya bacteria kwenye njia ya uzazi.
  • Kusafishwa kizazi mara kwa mara na matumizi ya kemikali kujisafisha ukeni, kitendo ambacho kinaharibu bacteria wazuri na kusababisha ukuaji wa bacteria wabaya na fangus
  • Matumizi ya kitanzi kwa ajili ya kupanga uzazi
  • Kuugua UTI mara kwa mara, na wanawake waliwahi kutoa mimba wapo kwenye hatari zaidi ya kupata PID
  • Uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya.
Hatua 4 Zifuatazo Zitakusaidia  Kuzuia Kupata Maambukizi Kwenye Njia Ya Uzazi (PID) Na Magonjwa Ya Zinaa
  1. Fanya ngono salama kwa kutumia kinga na kuishi na mpenzi mmoja mwaminifu.
    hii ni hatua muhimu ya kwanza na ya uhakika zaidi katika kuzuia kupata PID maana tayari tumeshaona hapo juu kwenye makala yetu njia kubwa ya kusambaa kwa maambukizi ni ni njia ya ngono. Kama ukichagua kuwa na wapenzi wengi basi hakikisha unavaa condom kwa kila tendo. Kama una mpenzi mmoja na kati yenu kuna ambaye kaugua basi hakikisheni mnaacha kufanya ngono mpaka pale mtakapotibiwa mkapona kabisa.
  2. Hakikisha unafanya vipimo kwa magonjwa ya zinaa na kuyatibu haraka iwezekanavyo
    wataalamu wa afya wanashauri kwamba watu walioko chini ya miaka ishirini na tano wafanye vipimo kila mwaka kwa magonjwa ya zinaa kama chlamydia. Wanawake wenye wapenzi wengi wanatakiwa kuonana na mtaalamu wa magonjwa ya wanawake(gynecologist) kwa vipimo kugundua uwepo wa vimelea vya magonjwa ya zinaa.ni muhimu kufanya vipimo mapema na kutibu mapema ugonjwa, kwa maneno mazuri ni kwamba kadiri unavochelewa kutibu magonjwa ya zinaa ndivyo unaongeza hatari zaidi ya kupata athari kubwa kwenye uzazi.
  3. Jikinge na maradhi ya bacteria na maambukizi mengine

Baadhi ya njia unazoweza kutumika kuzuia kutokea kwa maambukizi ni

  • Tumia sabuni zisizo na harufu kali(mild soap) kujisafisha- kuosha uke kwa kutumia sabuni zenye harufu kali na kemikali hufanya tishu za uke kututumka, kuharibu uwiano wa bacteria kenye uke na pia kupunguza tindikali iliyopo mpaka kupelekea kuongezeka kwa uchafu unaotolewa
  • Ukiwa kwenye hedhi tumia pedi zisizo na kemikali, pedi za asili zisizo na harufu kali. Hii itasaidia kuzuia ukuaji wa bacteria kwenye uke.
  • Hakikisha unaimarisha kinga yako ya mwili : unapokuwa na kinga imara basi unajikinga dhidi ya kushambuliwa na magonjwa ya zinaa.
  1. Epuka kujisafisha mara kwa mara ukeni. Kujisafisha kupita kiasi kunaharibu mpangilio wa kawaida wa bacteria kwenye uke(normal flora). Baadhi ya wanawake wanadhani kujisafisha sana husaidia kuondoa mambukizi, lakini ukweli ni kwamba uke uko na uwezo wa kujisafisha wenyewe. Kwahiyo unapotumia kemikali na spray kujisafisha unaua bacteria wazuri na kuongeza athari na ahatari ya kupata maambukizi.

YA WEWE KUZINGATIA NDIYO HAYA

Endapo utagundua kwamba unapata dalili za magonjwa ya zinaa kama tulivoelekeza hapo juu mfano MAUMIVU YA TUMBO CHINI YA KITUVU maumivu wakati wa kujamiiana, maumivu wakati wa kukojoa, hedhi kuvurugika, MAUMIVU MAKALI WAKATI WA HEDHI, na mengine, basi hakikisha unamuona Dactari mapema kwa ajili ya vipimo. Kama unashiriki ngono na mwenzi wako pia inashauriwa wote mpate vipimo na kutibiwa vizuri.

Muhimu kwa Wagonjwa wa PID

Kwa mwanamke mwenye changamoto ya PID, maambukizi ya bacteria na hedhi kuvurugika, tunashauri atumieTOP 8 CLEANSING POWDER kusafisha kizazi na kutibu maambukizi.TOP 8 CLEANSING POWDER  (TOP 8) ni MIMEA 3 iliyotengenezwa kitaalamu kwa kuzingatia uasili wa dawa kutatua changamoto za wanawake kama , harufu mbaya ukeni, muwasho,UTI, fangasi, PID na maambukizi ya bakteria

Pelvic Inflammatory disease-Standard Treatment Guidelines
TOP 8 CLEANSING POWDER Ndiyo suluisho la maradhi sugu ya zinaa


Pelvic inflammatory disease treatment naturally ▷ Legit.ng


  TOP 8 CLEANSING Powder utumika kwa siku 15. dawa hii utumika kwa muda wa siku 15, na baada ya hapo unakuwa umemaliza dose yako hii dawa umaliza moja kwa moja


Treat Pelvic Inflammatory Disease Naturally With These 5 Home ...


Dawa yetu ya TOP 8 Cleansing powderaina gharam sana Ni Tsh  65,000/=

Angalizo Unapotumia TOP 8 Cleansing Powder

  TOP 8 haifai kutumiwa na wajawazito. Usifanye tendo la ndoa wakati huo upo kwenye dozi na pia ukianza hedhi pumzika kutumia TOP 8 mpaka pale utakapomaliza hedhi.

  Whatsapp namba : 0757349219 kupata Huduma

Share and Enjoy !

WE TREAT BUT GOD CURE

0 0 0






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

YOU HAVE A BRIGHT FUTURE. IF YOU WILL GIVE YOUR EARTHLY LIFE TO JESUS

https://mbochiherbal.blogspot.com But if you contract HIV you need to think through what you need to change in your life and then set to work to rebuild your immune system

WATU WA KALE WALIAMINI TANGAWIZI NI TIBA ZAIDI MAANA ILITIUBU MARADHI 28

WATU WAKALE WALITUMIA ZAO LA TANGAWIZI KAMA TIBA KWA KUTIBU TAKRIBANI MAGONJWA 28 NA 100% WALIPONA Tangawizi (kwa Kilatini zingiberis rhizoma; kwa Kiingereza: ginger) ni mzizi wa mtangawizi. Umbo la tangawizi ni kama lile la mzizi wa manjano na yote miwili hutumika kama viungo katika chakula. TANGAWIZI NI TIBA KUBWA IKITUMIWA VEMA Tangawizi huwa na utomvu wenye mafuta na kampaundi zinazofanya ukali wake. Utafiti wa kisasa umegundua tangawizi inaweza kusaidia katika matatizo ya utumbo na kuzuia kutapika Tangawizi inatazamiwa kupunguza maumivu ya viungo vilivyoathiriwa na rumatizimu na homa ya baridi yabisi (arthritis) KWENYE ELIMU YA KALE WALITUMIA TANGAWIZI KUJENGA AFYA Katika elimu ya tiba ya kale tangawizi ilitazamiwa kuwa na tabia nyingi za kujenga afya, lakini matokeo mengi yanayodaiwa mwilini hayajathibitishwa kisayansi: Imedaiwa kuwa na uwezo ufuatao wa kitiba: 1. kuondoa sumu mwilini Sumu ni dutu yoyote inayoweza kuharibu kiasi kidogo shughuli za seli au inayo...

TIBA YA SHINIKIZO LA JUU LA DAMU

Shinikizo la juu la damu Shinikizo la juu la damu (HTN) au presha ya juu ya damu (pia huitwa shinikizo la mishipa ya damu , HBP), ni ugonjwa sugu ambapo nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa ni kubwa kuliko kawaida. Ongezeko hilo husababisha moyo kufanya kazi kupita kiasi ili uzungushe damu katika mishipa ya damu. Kwa kawaida halina dalili, ila likidumu lina madhara makubwa kwa afya. Shinikizo la juu la damu ndilo sababu kubwa (kihatarishi) ya upoozaji, mshtuko wa moyo (mashambulizi ya moyo), moyo kushindwa kufanya kazi, kutuna kwa ukuta wa mishipa (k.m., kutuna kwa ukuta wa aota au mkole), chujio la mshipa wa kupeleka damu kwenye moyo au peripheral arterial disease, na inasababishwa na ugonjwa sugu wa figo. Hata ongezeko la wastani la shinikizo la damu hupunguza matarajio ya muda wa kuishi. Kuna vipimo viwili vya shinikizo la damu, yaani systolic na diastolic: shinikizo au presha ya systolic ni kipimo cha damu ambacho kinapima nguvu ya msukumo wa damu katika mish...